ebook img

SOTERIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU WOKOVU PDF

154 Pages·2021·0.55 MB·Kiswahili
Save to my drive
Quick download
Download
Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.

Preview SOTERIOLOJIA: MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU WOKOVU

SOTERIOLOJIA MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU WOKOVU TEOLOJIA PANGILIFU-2 1 Hakimiliki © 2020 Daniel John Seni Chapa ya January, 2021 Msanifu: Eternal Word and Charity Publishing (EWCP). Dar es Salaam [+255-755-643-590] Mchapaji: Truth Printing Press. Dar es Salaam [+255764425704] ___________________________________ Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho hili inayoweza kuzalishwa tena, au kuboreshwa au kusambazwa kwa njia yoyote au kwa kubadilisha umbo au kunakili na kupeleka katika umbo lingine bila idhini ya mwandishi. _______________________________________ Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili Union Version (SUV). Tafsiri iliyotumika kwenye marejeleo yaliyokuwa kwenye lugha ya kiingereza si tafsiri rasmi; hivyo inaweza kuendelea kuboreshwa kwa kila chapa ya kitabu hiki. ________________________ Msambazaji Shekinah Mission Centre (SMC) [email protected] S.L.P 32807 Dar es Salaam +255 769 080 629 +255 787 907 347 Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya Msingi-Atlas/ at Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam TABARUKU Kwa wanazuoni wote wa teolojia i UTANGULIZI Huu ni mfululizo wa masomo katika uwanja wa “Teolojia Pangilifu” (Systematic Theology). Sasa tunashughulikia somo la Soteriolojia, yaani somo linalohusu “wokovu wa mwanadamu.” Siku hizi pengine inaweza kudhaniwa kwamba kila Mkristo anajua maana ya wokovu na upatikanaji wake. Watumishi wengi wasiopenda kujishughulisha huishia kusema “Yesu anaokoa” bila kufafanua maana ya sentensi hii nyepesi na rahisi sana. Ni kweli katika muktadha wa misiolojia tunaweza kutumia sentensi nyepesi kama hizi bila kuzitolea ufafanuzi kwa sababu wale tunaowaambia tunachukulia kwamba hawajui kitu chochote. ii Siku hizi kuna makanisa yanayojiita, “makanisa ya wokovu” ambayo hudai kuhubiri wokovu wa kweli. Hata hivyo, nimegundua mapungufu mengi katika mafundisho yao kuhusu wokovu kwa kudhania kwamba wokovu ni tukio la sekunde moja. Ama kwa hakika, wokovu ni mchakato; ingawa yawezekana michakato hiyo isipangiliwe vizuri na kuleta maana, lakini bado tunapaswa kujua kwamba wokovu ni mchakato. Mchakato wa kumwokoa mwanadamu unaanzishwa na Mungu mwenyewe na kumaliziwa pia na Mungu mwenyewe. Katika kitabu hiki, kwa namna ya upekee nimejaribu kufafanua kwa undani kuhusu michakato hiyo kwa kuzingatia ufafanuzi iii wa teolojia iliyoboreshwa (Reformed Theology) Kitabu hiki si kwa wale ambao wameshazaja akili zao mafundisho mbalimbali ya wokovu, na hivyo hawataki kubadilisha mwelekeo na kujifunza upya. Pia kitabu hiki si kwa wazembe, wasiopenda kushughulisha akili zao. Si kwa wale wanaopenda kutafuniwa tu, bali ni kwa wale ambao wanaweza kuvunja mifupa na kuelewa. Ninakutia moyo kwamba unaposoma kitabu hiki unahitaji kusoma katika hali ya utulivu, na kumwomba Roho Mtakatifu akusaidie ili uweze kuelewa zaidi na zaidi somo hili muhimu. Marejeleo mengi yaliyotumika katika kitabu hiki yanatokana na lugha ya Kiingereza, iv hivyo basi, kwa wale ambao wana uwezo wa kusoma Lugha ya Kiingereza wanashauriwa kupata baadhi ya nakala za vitabu hivyo kwa sababu ni muhimu sana. Yawezekana katika kitabu hiki ninaweza nisikubaliane na baadhi ya tafsiri ya kambi ya Teolojia Iliyoboreshwa kwa asilimia zote, lakini kwa kweli kwa sehemu kubwa inakubaliana na mafundisho halisi ya Neno la Mungu. v Yaliyomo TABARUKU ................................................. i UTANGULIZI .............................................. ii Yaliyomo ................................................... vi SURA YA KWANZA ..................................... 1 Maana ya soteriolojia ............................... 1 Kila Dini Hutafuta Wokovu ...................... 4 Hitaji la Wokovu kwa Mwanadamu .......... 7 Mpango wa Wokovu wa Mungu kwa Wokovu wa Mwanadamu ....................... 10 Mungu alijua mapema kila kitu ............. 12 Mpango wa Kusudi la Mungu la Milele .. 19 Wito wa Kupokea Wokovu...................... 21 SURA YA PILI ........................................... 25 MPANGILIO WA WOKOVU ........................ 25 SURA YA TATU ......................................... 34 KUCHAGULIWA MAPEMA NA KUITWA ..... 34 vi a. Kuchaguliwa .................................. 34 Dhana potofu kuhusu kuchaguliwa mapema ................................................ 42 Majibu kwa dhana potofu ...................... 44 Ni Wateule tu. ........................................ 46 b. Kuitwa ............................................ 55 Maswali fikirishi .................................... 66 SURA YA NNE .......................................... 67 KUZALIWA UPYA NA KUHESABIWA HAKI 68 a. Kuzaliwa Upya................................ 68 b. Kuhesabiwa Haki ........................... 75 SURA YA TANO ........................................ 88 TOBA NA UTAKASO ................................. 88 a. Toba ............................................... 88 b. Utakaso .......................................... 97 SURA YA SITA ........................................ 103 vii

See more

The list of books you might like

Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.