ebook img

Siasa ni kilimo. Mei, 1972 PDF

34 Pages·1972·0.656 MB·Swahili
by  coll.
Save to my drive
Quick download
Download
Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.

Preview Siasa ni kilimo. Mei, 1972

SIASA NI KILIMO TANU Gaylord JQ 3519 A8 T2236 SIASA NI KILIMO TANU RINGA. MEI. 1972 33 {3 -2%-77 TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION SIASA NI KILIMO “ Kwa miaka ijayo wananchi walio wengi wataendelea kuishi vijijini na kujipatia ri zikiyao kwa njia ya kilimo. Ardhi ndiyo msingi mkubwa wa maendeleo ya watu wetu na nchi yetu. Hatuna msingi mwi ngine. Kama hivyo ndivyo ni dhahiri kwamba kama maisha ya vijijini yasipo kuwa ya kijamaa nchi yetu haitakuwa ya kijamaa, hata kama viwanda, biashara, na siasa vina msingi wa kijamaa. Kwa sasa kitovu cha ujamaa wa Tanzania lazima kiwe vijiji na wakulima vijijini.” (Ujamaa Vijijini) (Halmashauri Kuu Iringa, Mei 1972) 1 SEHEMU YA KWANZA UMUHIMU WA KILIMO Kilimo chetu pamoja na ufugaji hakina budi kitoshelezemahitaji yafuatayo: 1. Kwanza, hakina budi kiwapatie wakulima chakula chao wenyewe. Ikiwa katika sehemuyo yote wakulima hawaku fanikiwa kupata chakula katika mwaka fulani, tunalazimika ama: (a) kupeleka chakula kutoka sehemu fulani, badala ya kukiuza chakula hicho na kupata fedha za kigeni; au (b) kutumia akiba yetu ya fedha za kigeni kununulia chakula kutoka katikanchizanje. Kwa kutumia njia yoyote katika hizo mbili, tutakuwa tumejipunguzia uwezo wetu wa kupata ama kuhifadhi fedha za 1 kigeni za kununulia vifaa kama mashine za kujengea viwanda vipya, matrekta, vifaa vya kuchimbia visima vya maji, malori,vyuma, n.k. 2. Pili, hakina budi kiwapatie chakula jamaa wote hawa wafuatao: (a) zaidi ya 44 kwa mia ya watuwetu walio watoto wa umri wa miaka 14 auchiniyake; (b) sehemu kubwa ya 9 kwa mia ya watu wetu walio wazee wa umri wa miaka 50 au zaidi. (Katika mwaka 1967 makundi hayo ma wili yalikuwa na watu 6,600,000 katika jumla ya wananchi wote 12,300,000); (c) watu wazima zaidi ya 450,000 na wake zao ambao hawalimi, lakini wanafanya kazi maofisini, serikalini, au mashuleni, au katika viwanda, au kazi za biashara, au katikamajeshi, n.k; 2 (d) watoto 5,300,000 watakaokuwa wamezaliwa kati ya 1967 na 1980, kama tukiendelea kuzaa na kuo ngezeka kwa kiasi kile cha 2.7 kwa mia kama ilivyo hivi sasa. 3. Tatu, hakina budi kuongeza ubora wa chakula tunachokula. Kwa wastani Watanzania wanaishi kwa miaka 40, ukilinganisha na wastani wa maisha ya Waingereza ambao ni miaka 70. Hali hii ya maisha mafupi inatokana zaidi na chakula kilicho hafifu; yaani chakula chetukinaupungufuwaproteni, vitamini, na viungo vingine vilivyo muhimu. Maana ya kuongeza ubora wa chakula ni kwamba haitoshi kupata chakula cha kujaza tumbo, lazima tupate chakula kinachohitajiwa hasa na mwili wa binadamu. Kwanza kabisa ni lazima tupate vyakula vinavyohitajiwa kwa ajili ya kujenga mwili. Vyakula hivi ni vya aina ya proteni, navyo ni kama nyama, maharage, samaki, karanga, maziwa na mayai. Pili lazima tupate vyakula tuna 3 vyohitaji kuimarisha afya ya mwili na kuwezesha kushindana na maradhi. Vyakula hivi ni kama mboga na matunda ya aina mbali mbali. Na tatu hatuna budi tupate chakula ambacho hucho mwa na mwili ili kuuwezesha kufanya kazi, kama vile mashini inavyochoma makaa au petroli na kuiwezeshakufanya kazi. Vyakula hivi ni kama mahindi, ngano, viazi, mtama, mhogo n.k. Kilimo chetu hakina budi kitupatie vyakula vya aina zote tatu, kwa kiasi cha kutoshanaubora wa kutosha. 4. Nne, kwa njia ya kilimo, lazima tupate mazao ya kuuza katika nchi za nje ili tupate fedha za kigeni tunazozi hitaji. Tusipofanya hivyo hatutaweza kununua kitu chochote kutoka katika nchi za nje ama kwa kazi za maendeleo ama kwa ulinzi wetu, ama hata kwa kuendeleza hali yetu ya sasa ya uchumi. Ilivyo sasa kati ya 85 kwa mia na 90 kwa mia ya bidhaa zetu tunazouza nchi za nje ni mazao ya kilimo, ama yaliyo 4 sindikwa kidogo ama yasiyotengenezwa kabisa. Na hata tukitaka kuendelea kupata thamani ile ile ya bidhaa zetu tunazouza nchi za nje, bado tutalazimika kuongeza kiasi cha mazao hayo kila mara, kwa sababu bei za mazao yetu katika masoko ya ulimwengu zinazidi kuanguka na zileza bidhaa tunazonunua zinazidi kupanda. Kwa mfano mwaka 1965 tungeweza kupata trekta moja kwa kuuza tani 5.3 za pamba yetu au tani 17.3 za mkonge wetu; leo trekta la namna ile ile litatugharimu tani 8 za pamba yetu au tani 42 za mkonge wetu ! 5. Na tano, kilimo chetu hakina budi kitupatie mazao kama pamba, kenaf, mbata n.k. tunayoyahitaji kwa viwanda vyetuwenyewe. 6. Kwa hiyo (a) lazima wakulima waeleweshwe uzitowa kazizao: wajivunie na kuelewa wajibu wao na watambue kuwa bilaya juhudi yao Taifa letu litaa nguka. Na (b) ujuzi wetu wa kilimo bora lazima uongezeke siku hata siku. 5

See more

The list of books you might like

Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.