ebook img

SANAA YA KUTOA NA KUPOKEA KATIKA MAHUSIANO PDF

54 Pages·2021·0.86 MB·English
Save to my drive
Quick download
Download
Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.

Preview SANAA YA KUTOA NA KUPOKEA KATIKA MAHUSIANO

[COMPANY NAME] [Company address] 1 Isaack Nsumba Toleo la kwanza June, 2021 @Haki zote zimehifadhiwa, hairuhusiwi kutoa sehemu yoyote ya kitabu hiki bila ruhusa ya mwandishi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote, taasisi au shirika lolote lile litakalodiriki kufanya hivyo. Isaack & Rebecca Nsumba P.O. BOX 674, Dodoma-Tanzania Phone: +255654722733 +255672356147 THE ARTS OF GIVING AND RECEIVING GIFTS IN RELATIONSHIP 2 SHUKRANI Ninamshukuru Mungu kwa namna alivyonifanya niwe mtu mwenye kugusa maisha ya wengi kupitia makala, vitabu na semina mbalimbali ambazo nimekuwa nikifanya kwa msaada wake, ninawashukuru wote ambao Mungu amekuwa akiwatumia katika namna ya moja kwa moja au isiyo na moja kwa moja kuhakikisha ile kiu iliyo ndani yangu ya kuona mabadiliko yanatokea kwenye maisha ya watu hasa kwenye eneo la ndoa na uchumi, ninamshukuru mpenzi wangu Rebecca kwa namna ambavyo amekuwa akinitia moyo na kuonesha kuamini pamoja nami katika kitu ambacho mungu ameweka ndani yangu kwaajili ya dunia. 3 YALIYOMO SHUKRANI ........................................................................... 2 YALIYOMO ........................................................................... 3 UTANGULIZI ........................................................................ 4 SURA YA KWANZA ............................................................... 7 SANAA YA UTOAJI ................................................................ 7 AINA ZA ZAWADI ................................................................... 9 UMUHIMU WA ZAWADI KATIKA KUKUZA, KUIMARISHA NA KUSITAWISHA MAHUSIANO. .............................................. 20 MAKOSA YA KUEPUKA WAKATI WA KUCHAGUA ZAWADI YA KUMPELEKEA MWENZI WAKO ...................................... 26 SURA YA PILI ..................................................................... 31 SANAA YA UPOKEAJI .......................................................... 31 DHUMUNI LA KUTOA .......................................................... 33 UMUHIMU WA KUTOA SHUKRANI KAMA ISHARA YA KUPOKEA ............................................................................. 36 NAMNA YA KUSHUKURU .................................................... 44 MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI UNATOA SHUKRANI KAMA ISHARA YA KUPOKEA HUDUMA .............................. 48 KUHUSU MWANDISHI ......................................................... 51 4 UTANGULIZI Kipekee kabisa mimi pamoja na Mpenzi wangu Rebecca tunasema ahsante kwa wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa msaada katika kuhakikisha tunaifikia hatma ya wito wetu tuliopewa na Mungu hapa duniani, tunatambua mchango wa kila mmoja iwe ni wa kifedha, kimawazo na hata wa kimaombi pia katika kuhakikisha tunawafikia watu wengi zaidi kupitia maarifa ambayo tumekuwa tukitoa kwenye mitandao ya kijamii, makanisani pamoja na kwenye makala mbalimbali na vitabu kama hiki. Ni matumaini yetu kuwa, kila atakaebahatika kusoma kitabu hiki hali ya hewa ya mahusiano yake itabadilika hasa kwenye eneo la kutoa na kupokea zawadi. Yamkimnin umekuwa ukitoa huduma Fulani kwa mwenzi wako lakini bado unaonekana kama hauugusi moyo wake sawasawa na vile 5 yeye anavyotaka au mwenzi wako amekuwa akijitahidi sana kutoa huduma Fulani huku akitegemea aina Fulani ya upokeaji na muitikio kutoka kwako lakini namna unavyoitikia inamvunja moyo na kumkatisha tamaa, kitabu hiki kimelenga kuwasaidia wapenzi wote kuboresha mahusiano yao kupitia kitgendo cha kutoa na kupokea iwe ni zawadi au aina Fulani ya huduma, ni kitabu ambacho kinalenga kuimarisha ngazi zote za mahusiano yawe ya kindugu, kikazi, kirafiki au ya kimapenzi (uchumba na ndoa) kwenye eneo la kujua namna ya kupokea vitu kutoka kwa watu. Usipojua namna ya kupokea unaweza jikuta unajifungia mlango wa kupokea vitu vingi hata Kama unastahiri kupokea, lakini pia ukiwa hujui namna ya kutoa katika namna inayomgusa uliemkusudia unaweza jikuta huduma yako inageuka kuwa kero na kupelekea mgogoro kati yako na mwenzi wako. 6 Ni kweli kwamba wahenga walisema “tenda wema (saidia, toa zawadi) ila usingoje shukrani”, kauli hii haimaanishi kuwa kwa sababu huwa hatungoji shukrani basi hatuhitaji kupokea shukrani kutoka kwa watu tuliowatendea mambo mazuri; isingekuwa rahisi kwa wahenga kusema “usingoje shukrani” ikiwa wanajua wazi kuwa hatuhitaji kushukuriwa, kauli hiyo inaashiria kuwa hitaji la msingi la kihisia la kila mwanadamu ni kujua jinsi kitu alichokifanya kwa mtu mwingine hasa ikiwa ni kizuri kilivyougusa moyo wake na hisia kwa ujumla. 7 SURA YA KWANZA SANAA YA UTOAJI MAANA YA ZAWADI, AINA NA UMUHIMU WAKE Tunapozungumzia kuhusu “zawadi” tunaznungumzia kitendo cha kuelezea hisia zako za upendo kwa mtu mwingine kupitia vitu, zawadi ni ishara, kiashiria au kielelezo cha thamani ya mpokeaji au nafasi aliyonayo mpokeaji ndani ya moyo wa mtoa zawadi. Watu wengi kwa kutokujua nguvu iliyojificha ndani ya zawadi wamekuwa wakilichukulia jambo hilo kiwepesi bila kulipa uzito unaotakiwa, lengo la kitabu hiki ni kukupandikizia ufahamu utakaokusaidia kulichukulia suala la zawadi katika namna ya uzito unaotakiwa na jinsi unavyoweza kuwa mbunifu katika kuchagua aina ya zawadi inayoendana na kile unachotaka mwenzi wako ajue baada ya kupokea zawadi yako. 8 Lengo la kutoa zawadi ni kufanya mawasiliano kati ya mioyo yenu miwili au kuwasilisha aina Fulani ya hisia kwa mwenzi wako (the primary purpose of giving a gift is to communicate your feelings to your spouse). Ndani ya zawadi yoyote ile kuna ujumbe umebebwa na mpokeaji itakuwa rahisi kuupokea bila hata mtoaji kufungua kinywa chake na kusema, hivyo itakuhitaji ubunifu wa hali ya juu zaidi ili ujumbe utakaopokelewa na mpokeaji baada ya kumpatia zawadi uendane na kile ulichokusudia. kama suala la utoaji lisipofanyika kwa umakini na kwa ubunifu mkubwa basi zawadi inaweza ikatumika kupeleka aina ya ujumbe ambao haukukusudiwa na mtoaji wa zawadi. 9 AINA ZA ZAWADI Katika kuangalia aina za zawadi ni muhimu kwanza tuchunguze aina za upendo, kwani kupitia hizo ndipo tutaweza kubaini aina za zawadi kwa sababu aina ya zawadi inasukumwa na aina Fulani ya upendo, yaani zawadi ni alama inayosimama kuwakilisha aina Fulani ya mahusiano ambayo yamejengwa juu ya aina Fulani ya upendo. 1. UPENDO WA AGAPE - UPENDO WA MUNGU. (Godly Love) Agape ni aina ya upendo wa ki-Mungu, utendao kazi ndani ya mtu pasipo masharti yoyote au sababu yoyote. Ni upendo usioangalia hali ya nje ya mtu. Ni nguvu au uwezo wa mvuto wa Ki-Mungu utendao kazi ndani ya mtu, kumwonyesha mtu mwingine wema wa Mungu bila kujali hali yake yoyote. Ni upendo usio na sababu yoyote; unampenda mtu kwasababu tu unatakiwa kumpenda, nukta. Hakuna sababu nyingine. 10 Kwa kingereza wanasema “unconditional love”. Aina hii ya upendo; agape, ni kama ule aliotuonyesha Mungu kwa kutupenda. Neno la Mungu linasema ‘Mungu alitupenda tungali wenye dhambi’, yaani bado tuna dhambi, madhaifu na bado akatupenda (Rum 5:8) ili atuokoe na mauti itokanayo na uasi kwa Mungu. Imeandikwa katika biblia kwamba Mungu aliupenda ulimwengu wenye kila aina ya uovu, uasi na uchafu (Yoh 3:16, Rum 1:28- 32) na akamtoa Kristo afe kwa ajili yetu, ili tuokolewe. Kwahiyo, alitupenda bila kujali uchafu na uasi tuliokuwa nao. Huo ndio upendo wa agape. Sifa kuu tatu (3) za Upendo wa ki-Mungu (Agape). i. Hauangalii hali ya mtu ya nje. ii. Hauna masharti yoyote ya kupenda. iii. Hauna kipimo au kiwango cha kupenda. iv. Hauna mwisho au kikomo cha kupenda. 11 2. UPENDO PHILEO – UPENDO WA KIRAFIKI. (Friendship Love) Phileo ni upendo wa kirafiki. Huu ni upendo wa tofauti kidogo na upendo wa agape. Phileo ni upendo wenye sababu. Kiingereza wanasema ‘conditional love’. Ni upendo wenye sababu. Huu ndio upendo unaokuwepo kati ya marafiki. Phileo ni upendo unaoshikiliwa na kishikizo/kifungo cha ‘masharti’ fulani au ‘sababu’ fulani. Mtu huwa rafiki wa mtu fulani ‘kwasababu’ fulani. Kuna mazingra yamewafanya watu fulani kuwa marafiki. Mazingira hayo au masharti fulani yakivunjika kati yao, basi upendo ulio kati yao huyeyuka na urafiki wao huvunjika. Aina hii ya upendo wa phileo ni kama ile ambayo Yesu anaisema katika kitabu cha Yohana 14:21,23. Anasema kwamba ‘mtu akinipenda, Baba atampenda, nami na Baba tutakuja kufanya makao ndani yake’. Huu ni upendo tofauti na ule unaotajwa katika Yohana 3:16 na Warumi 5:8 ambao unasema 12 Mungu alitupenda tungali wenye dhambi pasipo masharti yoyote. Yaani, kwa upendo agape, Mungu hakujali hali zetu za nje wala masharti yoyote. Lakini kwa upendo phileo, Mungu anaangalia kwanza kama mtu atatimiza masharti aliyoyaweka, kisha ndipo na yeye Mungu anaachilia upendo phileo kwa mtu huyo, anakuwa rafiki yake. Mahali pengine Yesu alisema kwa wanafunzi wake kuwa ‘siwaiti ninyi tena watumwa bali marafiki.’ Hilo neno ‘tena’ linamaanisha kwamba, baada ya kukaa na wanafunzi wake kwa muda fulani, waliweza kufikia kiwango Fulani cha masharti alichokitaka Bwana, hata sasa wamefika katika ngazi wa kuwa marafiki wa Yesu na sio watumwa tena. Ndio maana imeandikwa pia katika kitabu cha Mithali 8:17 kuwa, ‘ninawapenda wale wanipendao …’ Hivyo phileo ni upendo wenye masharti na sababu. Rafiki wa mtu husema ‘nampenda mtu Fulani, rafiki yangu kwasababu…’ Labda kwa sababu wanasoma wote au kwasababu 13 alimsaidia katika eneo fulani au kwasababu anatabia fulani au kwasababu wanatoka kijiji kimoja, n.k. Sifa kuu tatu (3) za Upendo wa kirafiki (Phileo). i. Unaangalii hali ya mtu ya nje. ii. Una masharti yoyote ya kupenda. iii. Una kiwango au kipimo cha kupenda. iv. Una mwisho au kikomo cha kupenda. 3. UPENDO STORGE– UPENDO WA KIFAMILIA. (Family Love) Upendo storge ni upendo wa kifamilia, ni upendo unaotokana na damu moja ya undugu. Ndugu wa damu moja hata kama hawapatani au wemegombana, bado ndani yao kuna upendo wa kindugu. Fikiria; mtu na mdogo wake wakiwa wamegombana sana na 14 kutupiana mito ya makochi na vitabu vyote vya kwenye shelfu za kabati, baadaye, mmoja akimkuta ndugu yake anaonewa au anagombana au anapigwa na muuza machungwa wa mtaani, huyu ndugu yake kwa vyovyote ataguswa tu, ataonyesha kujali tu au anaweza hata kuweka tofauti zao pembeni na kuingilia kumsaidia. Msukumo huo au mvuto huo, ni mvuto unaotokana na viini vya upendo wa kifamilia unaowafungamanisha watu wa damu ya familia moja au ukoo mmoja. Upendo wa kindugu, storge unafanana kwa sehemu na ule upendo wa ki-Mungu wa agape. i. Hauangalii hali ya nje ya mtu. ii. Hauna masharti ya kupendwa. iii. Hauna kikomo au mwisho wa kupendwa. Tofauti yake moja kubwa na upendo wa agape ni kwamba, upendo wa kindugu una kiwango au kipimo cho kupenda. Ndugu wanapendana lakini kwa viwango tofauti;

See more

The list of books you might like

Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.