ebook img

Maisha ya ujamaa PDF

56 Pages·1969·4.699 MB·Swahili
by  coll.
Save to my drive
Quick download
Download
Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.

Preview Maisha ya ujamaa

JQ 3515 .T164 TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION MAISHA YA UJAMAA see C h o INGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION MAISHA YA UJAMAA Bei 1/50 Tanganyika Ifrican National Ilsvos . MAISHA YA UJAMAA J Q 3515 .T 164 INDIANA UNIVERSITY LIBRARIES BLOOMINGTON Makao Makuu ya TANU Dar es Salaam 21 N Y 4-3.75 MAISHA YA UJAMAA Ili tuwe wajamaa halisi hatuna budi tuishi kljamaa; hakuna anayeweza kuwa mjamaa, na huku anaishi maisha ya peke yake. Kuishi kijamaa ni kukaa pamoja na wengine, na kufanya kazi pamoja, kwa manufaa ya wote. Kuishi na kufanya kazi pamoja si jambo rahisi, hasa katika siku za mwanzo, ingawa sababu za kuishi katika kijiji cha ujamaa ni rahisi kuzieleza. Watu wengi wanaoishi pamoja kwa kuheshimiana na kwa mpango . maalum wa kazi wana nguvu zaidi kuliko mtu pekee. lli juhudi ya kuishi na kufanya kazi pamoja ifanikiwe, lazima wote wanaohusika wazielewe tokea mwanzo shabaha zao, na wawe na shauku ya kuzitimiza. Jambo 1 1 muhimu sana litakalofanya vijiji vya ujamaa viendelee ni wanakijiji wenyewe kuelewa shabaha zao, na kuwa na ujuzi wa kuzitekeleza. Kusema kweli kile kitendo cha watu waliokuwa maskini na wasio na elimu kukusanyika pamoja haki wafanyi wawe wakulima matajiri zaidi, na wenye ujuzi Bali kitendo hicho cha kukusanyika pamoja bora. huwapa uwezekano wa kufanya kazi zaidi katika juhudi zao za kupambana na Umaskini na Ujinga. Ni wajibu wa TANU na Serikali kufanya kila juhudi ya kuwaeleza watu kuwa mipango ya kuishi pamoja huleta maisha bora zaidi. Na haitoshi kuwaeleza tu, bali pia kuwaonyesha kwa mifano iliyo wazi jinsi faida hizo zitakavyopatikana. Lakini kwa vyo vyote vile ni juhudi za wanakijiji wenyewe tu zinazoweza kuyatimiza yale yanayoweza kutendeka. Hapana sababu ya kuanzisha au kujiunga na kijiji cha ujamaa ila kwa nia ya kutaka kuleta mabadiliko, au mapinduzi. Mapinduzi yo yote ni ya mtu binafsi, hakuna 1 anayeweza kumfanyizia mwenziwe mapinduzi. Vijiji vya Ujamaa ni vya wale waliochoshwa na umaskini, na kukasirishwa na ujinga na maradhi. Vijiji vya Ujamaa ni kwa wanaume, wanawake na watoto, walio na hamu ya maisha mapya, wakitambua kuwa maisha hayo mapya hayawezi kujengeka isipokuwa kwa kugeuza kabisa maisha ya zamani, na sasa wako tayari kufanya kazi kutwa kucha ili kujiondosha katika hali yao ya unyonge. Watu wanaoishi katika Kibutzi, yaani vijiji vya ujamaa vya huko Israeli, au katika 'Kommune', yaani vijiji vya Ushirika huko China, walifanya kazi kwa juhudi kama hiyo, na wakagundua kuwa matokeo yake yalikuwa ni ya kuridhisha sana. Kuanzisha kijiji cha Ujamaa ni kuanzisha vita, kupigana na Umaskini, Ujinga na Maradhi. Ili kushinda umaskini, ujinga na maradhi wanakijiji hawana budi kupigana vita vikali. Kama watu katika kijiji cha Ujamaa hawakushirikiana kijeshi katika juhudi zao, wakitumia akili na taratibu nzuri, wasitu maini kushinda katika vita hivi. Wakazi wa kila kijiji cha Ujamaa lazima wawe jeshi la watu linalopigana vita vya watu; vita vya kutafuta amani na maisha bora. Ni vita vikali, na ili kushinda katika vita hivyo unahitajiwa ushujaa na juhudi nyingi. Wanaoweza kujenga vijiji vya Ujamaa ni watu wale wanaoamini mipango ya kijamaa, na kujitolea kujenga maisha ya kijamaa kwa faida ya watu wote. Maneno haya, kujitolea, kuelewa, kujua, kushiri kiana, kuwa na hakika, utaratibu wa kazi, ushujaa, juhudi, utundu, ni maneno mazuri; lakini yana maana gani? Yana maana gani kwa kazi za watu wanaoishi katika kijiji cha Ujamaa, siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi, mwaka baada ya mwaka, ili kujipatia riziki na maisha bora? Yana maana gani kwa wazee waliokwisha fanya kazi maisha yao yote; kwa wanaume, wanawake, watoto; kwa vijana wenye afya na ari, na 2 wasichana? Yana maana gani kwa ardhi, nyumba, majembe, mpunga, mbegu, jua kali, mahindi, pamba, kahawa, ng'ombe, mbuzi na kuku? Maswali haya haya wezi kujibiwa ila kwa vitendo. Tutayaeleza maneno hayo, ili tujiandae kwa vitendo. UMOJA Umoja huzaa nguvu. Umoja ni nguvu; utengano ni udhaifu. Haya ndiyo maneno yaliyotuongoza katika kupigania Uhuru! Mpaka sasa yangali na maana. Ingefaa kila kijiji cha Ujamaa kuyaandika maneno haya kwa herufi kubwa katika ukumbi wa mkutano. Umoja ndio msingi mkuu wa maisha ya kijiji cha Ujamaa. Lakini umoja huu unaweza kujengwa, kuhifadhiwa na kudu mishwa namna gani? Umoja unategemea watu kuelewana, kuheshimiana na kuaminiana. Wale watu wanaoanza kijiji cha Ujamaa lazima wajuane vema, na lazima wajadili kiasi cha kutosha kitu cho chote wana chotaka kufanya, ili waweze kkuuaammiinniiaannaa.. Lazima waelewe wazi kwamba: 1 . Juhudi tunazofanya pamoja ni zetu wote, kwa hivyo wajibu ni wetu wote. Wajibu wa kwanza uwe kati yao wenyewe, 2. wala siyo kwa ndugu walio nje ya kijiji. 3. Wote wako tayari kufanya kazi kwa bidii na kuvumilia hata wakati wa shida kubwa. Mtu mvivu, yule anayedharau madaraka yake, mlevi, au mgomvi, hawa wote si rahisi kuwa nao katika . kijiji cha Ujamaa. Ikiwa mtu ana walakini katika tabia H yake, itafaa wakazi wa kijiji cha Ujamaa wafikirie sana kabla ya kumkaribisha kuishi nao, na hata wakimka ribisha lazima wawe na utaratibu mzuri wa kumchunga, na kama lazima wawe na muda wa kuchunguza tabia yake kabla hajakubaliwa. Vijiji vingi vya Ujamaa 3 N anayeweza kumfanyizia mwenziwe mapinduzi. Vijiji vya Ujamaa ni vya wale waliochoshwa na umaskini, na kukasirishwa na ujinga na maradhi. Vijiji vya Ujamaa ni kwa wanaume, wanawake na watoto, walio nahamu ya maisha mapya, wakitambua kuwa maisha hayo mapya hayawezi kujengeka isipokuwa kwa kugeuza kabisa maisha ya zamani, na sasa wako tayari kufanya kazi kutwa kucha ili kujiondosha katika hali yao ya unyonge. Watu wanaoishi katika Kibutzi, yaani vijiji vya ujamaa vya huko Israeli, au katika 'Kommune', yaani vijiji vya Ushirika huko China, walifanya kazi kwa juhudi kama hiyo, na wakagundua kuwa matokeo yake yalikuwa ni ya kuridhisha sana. Kuanzisha kijiji cha Ujamaa ni kuanzisha vita, kupigana na Umaskini, Ujinga na Maradhi. Ili kushinda umaskini, ujinga na maradhi wanakijiji hawana budi kupigana vita vikali. Kama watu katika kijiji cha Ujamaa hawakushirikiana kijeshi katika juhudi zao, wakitumia akili na taratibu nzuri, wasitu maini kushinda katika vita hivi. Wakazi wa kila kijiji cha Ujamaa lazima wawe jeshi la watu linalopigana vita vya watu; vita vya kutafuta amani na maisha bora. Ni vita vikali, na ili kushinda katika vita hivyo unahitajiwa ushujaa na juhudi nyingi. Wanaoweza kujenga vijiji vya Ujamaa ni watu wale wanaoamini mipango ya kijamaa, na kujitolea kujenga maisha ya kijamaa kwa faida ya watu wote. Maneno haya, kujitolea, kuelewa, kujua, kushiri kiana, kuwa na hakika, utaratibu wa kazi, ushujaa, juhudi, utundu, ni maneno mazuri; lakini yana maana gani? Yana maana gani kwa kazi za watu wanaoishi katika kijiji cha Ujamaa, siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi, mwaka baada ya mwaka, ili kujipatia riziki na maisha bora? Yana maana gani kwa wazee waliokwisha fanya kazi maisha yao yote; kwa wanaume, wanawake, watoto; kwa vijana wenye afya na ari, na 2

See more

The list of books you might like

Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.