ebook img

MABADILIKO YANAYOUMIZA NDANI YA KANISA PDF

81 Pages·2020·0.731 MB·Kiswahili
Save to my drive
Quick download
Download
Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.

Preview MABADILIKO YANAYOUMIZA NDANI YA KANISA

MABADILIKO YANAYOUMIZA NDANI YA KANISA D.J. SENI ii Hakimiliki © 2020 Daniel John Seni [email protected] Msanifu: Eternal Word and Charity Publishing (EWCP) Dar es Salaam [+255-755-643-590] Mchapaji: Truth Printing Press. Dar es Salaam [+255764425704] Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya kitabu hiki inaweza kuzalishwa tena bila ruhusa ya Mfasiri isipokuwa kwa mhakiki ambaye anaweza kunukuu vifungu vifupi vifupi katika hakiki zake; Wala sehemu yoyote ya kitabu hiki hairuhusiwi kuwekwa katika umbo lingine bila kibali cha mwandishi _______________________________________ Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili Union Version (SUV) kinapatikana Shekinah Mission Centre (SMC) [email protected] S.L.P 32807 Dar es Salaam +255 769 080 629 +255 787 907 347 Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya Msingi-Atlas/ at Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam Tabaruku Kwa wazazi wangu. Kwa Mwl. Boyeon Lee Kwa Mama S.N. Choi Mungu amewatumia kwa namna ya pekee watu hawa kwa kupokezana majukumu ya kunilea, kunifundisha, na kunipatia msaada; kila mmoja kwa wakati wake na kwa juhudi kubwa. Mungu awabariki sana. i Utangulizi Katika mataifa ya mengine siku hizi huwezi kuwa mchungaji wa kanisa linalojitambua ukiwa huna angalau Elimu ya Sekondari na kumaliza seminari. Katika nchi zingine, uchungaji imeorodheshwa kuwa mojawapo ya kazi zinazotambuliwa ndani ya serikali. Ni mojawapo ya kazi ambayo mtu lazima awe na maarifa ya Mungu na ya kidunia. Kinyume chake, katika mataifa mengine, mtu akiweza kunena kwa lugha tu, anakabidhiwa kundi. Ndiyo! Naamini katika uongozi wa Roho Mtakatifu katika kuongoza kanisa; wenye elimu na wasio na elimu ni sawa tu. Na wakati mwingine wasio na elimu yoyote wanaweza kuongoza kanisa vizuri kuliko wenye elimu. Hata hivyo, itakuwa ni kazi kubwa sana yenye kuchosha, kwa sababu mambo mengi unaweza kuyafanya kama uko gizani. Kwa kuzingatia uhitaji wa elimu ya uongozi ndani ya kanisa; uwe na elimu, ama usiwe na elimu, kitabu hiki kinakufaa kwa sababu nimekiandika katika mazingira ya uzoefu na mazoezi; kitamsaidia kiongozi yeyote ndani ya kanisa kuwa mwajibikaji ikiwa ataamua kukitumia vizuri, na kufuata maelekezo yake. Katika kitabu hiki, nimejaribu kujadili kwa kina mambo muhimu ambayo mtumishi wa Mungu akiyafanya ndani ya kanisa kuna uwezekano mkubwa wa kubadilisha kundi lake. Nimezungumzia mabadiliko ya kulifanya kanisa liwe ni kanisa hai mbele za Mungu likiwa linatimiza Utume Mkuu. Ni kweli kwamba Mungu ndiye huleta mabadiliko ndani ya kanisa, lakini ukweli huu hauondoi jukumu la kiongozi wa kanisa; mchnungaji, mzee, mwinjilisti, shemasi, mkuu wa idara, pamoja na kila muumini ndani ya kanisa. Pamoja na juhudi kubwa za viongozi wa kanisa, kuna uhitaji wa kanisa zima kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kanisa, ili kanisa likue kwa pamoja. Mch. Daniel John Seni Shekinah Presbyterian Church in Tanzania, Dar es Salaam Desemba, 2020 ii YALIYOMO Tabaruku ...................................................................... i Utangulizi .................................................................... ii YALIYOMO .................................................................. iii SURA YA KWANZA ....................................................... 1 TAMBUA DHANA YA KUPINDUA ULIMWENGU ................. 1 SURA YA PILI ............................................................... 8 TAMBUA AINA YA WASHIRIKA ULIO NAO ......................... 8 1. Washirika Wanaokataa Uhalisia wa Kanisa lao ........ 9 2. Washirika waliojikinai............................................ 11 3. Washirika walalamikaji .......................................... 12 4. Washirika wakosoaji .............................................. 14 5. Washirika Walioridhika na Hali ya Kanisa ............. 15 6. Washirika Tegemezi ............................................... 17 SURA YA TATU .......................................................... 19 TAMBUA MAMBO YA MSINGI KUANZA NAYO ................. 19 1. Maombi Yasiyokoma .............................................. 19 2. Fikiria mambo makubwa kuliko uwezo wako ......... 21 3. Kubali Ukweli na Ukabili Ukweli ............................ 25 4. Jifunze kwa Wengine. ............................................ 31 5. Kubali Kulipa Gharama ......................................... 32 6. Pambana na Tabia Zinarudisha Maendeleo ........... 37 7. Kuwa Sauti ya Matumaini na Maono ..................... 42 8. Tarajia Upinzani Kwenye Mabadiliko ..................... 48 iii 9. Shughulika na Mahitaji ya Watu ........................... 53 10. Kuthamini Watu Wanaokuunga Mkono ................. 58 11. Kubali bila Majuto wengine Waondoke................... 59 12. Zingatia Uwezo wa Washirika ................................ 61 13. Mfanye Kila Mshirika Awe Shahidi .......................................... 62 Historia ya Mwandishi ............................................................... 72 iv SURA YA KWANZA TAMBUA DHANA YA KUPINDUA ULIMWENGU Tuanze kwa kusoma Matendo ya Mitume 17:6 “na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako.” Na pia Matendo ya Mitume 5:28 “akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.” Katika mistari tuliyosoma, tunaona maneno yanayoshahibiana; kwamba watu ambao wanazungumziwa katika Maandiko haya walifanya mabadiliko makubwa. Katika ule mstari wa kwanza, tunaona maneno haya "watu hawa waliopindua ulimwengu wamefika huko nako." Ni kauli ambayo inaonyesha kwamba, wanafunzi wa Yesu Kristo, walikuwa wamefanya mabadiliko makubwa, mabadiliko ambayo ni ya kupindua ulimwengu. Mabadiliko ya namna hii hayakuwa mepesi hata kidogo. Tunajua wazi kwamba Bwana wetu Yesu Kristo alipokuwa karibu na kuondoka, aliwaagiza wanafunzi wake akawaambia, ya kwamba Roho Mtakatifu atakapokuja kuwatia nguvu. Anasema katika matendo ya mitume 1:8 kwamba, "nanyi mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu." Ahadi ya Bwana wetu Yesu 1 Kristo ilitimia katika matendo ya mitume sura ya pili. Kuanzia hapo tunaona wanafunzi wanafanya kazi kubwa. Makundi ya aina mbili yalikuwepo: kundi la kwanza kundi la mitume, na kundi la pili, kundi la wanafunzi wa Yesu kwa ujumla; hawa wote walifanya kazi kwa bidii. Kazi yao ilikuwa inaeleweka, na ndiyo maana katika matendo ya mitume sura ya 5:28 tunaambiwa kwamba walikuwa wameijaza Yerusalemu kwa mafundisho yao. Mafundisho ya aina gani hayo? Ni mafundisho ya ufufuo wa Yesu Kristo. Wakaanza kuwa tishio kwa watawala wa wakati huo. Tunaona wakuu wa baraza la Kiyahudi la Sanhedrini linaanza kukutana kujadili hoja mafundisho ya wanafunzi wa Yesu. Wakawaita Petro na Yohana na kuwaambia waache mara moja kuhubiri kwa jina la Yesu kwa sababu wanaleta doa kwa taifa la Israeli kwa kuonesha kwamba watu hawa walimuua Yesu. Petro na Yohana wanasema hatuwezi kunyamaza kwa sababu “hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Ni jina la Yesu peke yake. Jina lenye kubadilisha. Jina lenye kuokoa. Jina linaloponya. Ni Yesu peke yake ambaye alikuwa amevamia ulimwengu kwa ajili ya kuleta mabadiliko mioyoni mwa watu. Ama kwa hakika shughuli ilikuwa pevu. Roho Mtakatifu aliyekumo ndani ya mitume, hakuwaruhusu kunyamaza. Tukisoma habari za Mtume Paulo katika utumishi wake tunaweza kujifunza mambo mengi. Kupindua ulimwengu halikuwa jambo jepesi kama ambavyo leo tunaweza kudhania. Kuwaendea watu wasio na ufahamu wowote kuhusu Kristo haikuwa kwa nguvu zao wenyewe bali Roho Mtakatifu aliwatumia watumishi hawa. Kama tunavyojua, mtume Paulo kabla ya kuokoka alikuwa mtu aliyejitolea kukomesha Ukristo kama ibada ya uwongo hadi, alipokutana na Yesu Kristo. Baada ya siku hiyo, aliamua kujitolea 2 kwa nguvu zake zote kutangaza Injili ya neema ambayo ilibadilisha maisha yake. Paulo anasema kwamba alikuwa amehesabu kama hasara kila kitu maishani mwake ambacho hapo awali kilikuwa faida kwake kwa kutazama thamani kubwa ya kumjua Kristo Yesu Bwana wake (Fil 3: 8). Kwa sababu ya kujua thamani hiyo, mtume Paulo alitaka watu wengine pia wajue thamani ya Kristo kwa; kumwamini na baada ya kumwamini wawafanye na watu wengine waamini. Kama matokeo ya kumjua Yesu Kristo kibinafsi, Paulo alisema kwamba alifanya kila kitu kwa ajili ya Injili (1 Kor. 9:23). Alipigwa huko Filipi, na badala ya kupumzika, alisafiri kilometa 160 kwenda Thesalonike, akaingia katika sinagogi, akaanza kufundisha kuwa Yesu ndiye Kristo. Alipolazimishwa kuondoka Thesalonike, alihamia Beroya na kufanya vivyo hivyo! Mtu huyo hakuwa akizuilika katika kujitolea kwake kuhubiri injili ya Kristo! Alikuwa anaongoza mabadiliko ya kupindua ulimwengu mzima. Alikuwa na ndoto ya kufikia ulimwengu mzima. Nguvu iliyombadilisha. Nguvu ya Roho Mtakatatifu ilikuwa inamsukuma Paulo kubadilisha ulimwengu mzima. Kupindua ulimwengu. Watu wa namna hii ni wachache sana; lakini miongoni mwa wachache ni wewe! Wewe unayeishi katika ulimwengu wa sasa unaweza kufanya mabadiliko makubwa kuliko aliyofanya Paulo ikiwa tu utakubali Bwana akutumie katika kazi yake. Bwana Yesu anatafuta watu ambao watapindua ulimwengu wao. Tunaposema kupindua ulimwengu hatumaanishi kwamba tunataka kuteka serikali zilizopo madarakani, kazi yetu ni moja tu; kuhakikisha kwamba tunawafikia watu wengine kwa ajili ya Injili. Si kuwafikia tu 3

See more

The list of books you might like

Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.