ebook img

Kamusi ya Tiba PDF

304 Pages·2003·20.051 MB·Kiswahili (Swahili); English
Save to my drive
Quick download
Download
Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.

Preview Kamusi ya Tiba

ENTTS ae :hw AA ot | REMOTE | STORAGE eEeWi<ea s2Nap a n e sA Waandishi: _A.M.A. Mwita H.J.M. Mwansoko LIBRARY Michigan State University anEe E Eeeee KAMUSI YA TIBA ¥, H.J M Mwansoko TAASISI YA UCHUNGUZI WA KISWAHILI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam S.L.P. 35110 Dar es Salaam Simu:022-2410757 Barua-e:[email protected] Webu:http//www.udsm.ac.tz/ikr © AM.A Mwita pi \ H.J.M. Mwansoko Chapa ya Kwanza 2003 ISBN 9976 911 65 3 Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga kunakili, kupiga chapa au kukitoa kitabu hiki au sehemu ya kitabu hiki kwa njia yoyote ile bila idhini ya Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 9057184 DIBAJI Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwapongeza waandishi vya kamusi hii, Prof. H.J.M Mwansoko na Dkt. A.M.A. Mwita kwa kuamua kutunga Kamusi ya Tiba ya Kiingereza- Kiswahili. Uamuzi wa Profesa Mwansoko, ambaye ni mtaalamu wa uundaji wa istilahi, na Dkt. Mwita, ambaye ni bingwa katika taaluma ya udaktari, sio kwamba unachangia tu jitihada za kuikuza lugha ya Kiswahili katika nyanja mbalimbali, bali pia ni mchango mkubwa katika jitihada za dhati zinazofanywa na asasi na wataalamu wazalendo za kukiandaa Kiswahili kushika hatamu za uongozi katika ufundishaji wa taaluma katika viwango mbalimbali vya elimu hapa nchini. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, imeichukulia kazi hii kwa uzito mkubwa. Taasisi, ikiwa ni asasi iliyopewa dhamana ya kufanya utafiti katika nyanja zote za lugha ya Kiswahili, ikiwa ni pamoja na uandikaji wa kamusi mbalimbali, inaona uchapishaji wa kamusi hii kama ushindi mkubwa katika jitihada zake za kutimiza dhamana iliyopewa. Ili kuhakikisha kuwa kazi inayotolewa iko katika kiwango cha juu cha ubora, Taasisi iliipitia kazi hii kuona kama kanuni za uandishi wa kamusi zimezingatiwa. Zaidi ya hayo, Taasisi iliamua kuipeleka kazi hii kwa wataalamu wa masuala ya uganga ili waweze kuipitia. Maoni yao yalizingatiwa na kuingizwa katika kazi hii. Lugha yoyote ile inaongeza wingi wa msamiati na istilahi zake pale inapopewa nafasi ya kutumika katika nyanja mbalimbali. Lugha isipopewa nafasi kubwa ya matumizi katika nyanja mbalimbali, msamiati wake unakuwa finyu. Hata hivyo, mara tu nafasi ikitolewa, lugha hujiundia msamiati na istilahi zake ili kukidhi haja ya matumuzi iliyojitokeza. Kwa kuwa tangu wahenga na wahenga, Kiswahili hakikuwa kimepewa nafasi kubwa ya kukitumia katika taaluma ya uganga, uhaba wa msamiati na istilahi za fani hii umejitokeza wakati wa kutunga kamusi hii ya tiba. Kamusi hii ya tiba ni ya Kiingereza Kiswahili. Kwa maana ya kwamba kamusi imeanza na orodha ya istilahi katika Kiingereza kisha kutafuta visawe vyake katika Kiswahili. Ziko baadhi ya istilahi za uganga za Kiingereza zimepata visawe vyake katika Kiswahili. Lakini kuna baadhi hazikuwa na visawe vyake. Kwa zile istilahi ..$. aa yanaweza kuelezea dhana zinazokusudiwa. Njia ya tatu ni kutoa maelezo tu ya dhana husika kwa Kiswahili fasaha. Utaratibu wa kuzitumia njia zote hizi tatu katika kutunga kamusi sio rahisi. Mwandishi anatakiwa kuwa mdadisi, mbunifu, makini, na mvumilivu. Zaidi ya hayo anatakiwa kutumia muda wake mwingi katika kufanya utafiti wa maktabani na uwandani. Kutokana na ugumu huo, ndio maana waandishi wa kamusi hii wamechukuwa takribani nusu mwongo katika kuiandika kamusi. Kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, tunapenda kuwapongeza sana kwa kazi kubwa waliyoifanya. Kamusi hii ni ya uwanja wa tiba na uuguzi. Kwa hiyo sio kamusi kwa ajili ya watumiaji wa kawaida wa lugha ya Kiswahili. Ni kamusi ambayo itawafaa sana wale walio katika uwanja wa uganga na uuguzi. Ijapokuwa istilahi na lugha iliyotumiwa humo ni Kiswahili, lakini yale yanayosemwa yataeleweka zaidi na watumiaji wa uwanja huo. Kwa hiyo, ni kamusi ambayo itawafaa zaidi waganga, wauguzi, mabingwa katika taaluma ya uganga na uuguzi, walimu na wanafunzi wa uganga na uuguzi. Ijapokuwa kimsingi hivyo ndivyo mambo yanavyotarajiwa kuwa, bado nashawishika kusema kuwa wazungumzaji wa Kiswahili wa kawaida na wale ambao ni wataalamu katika nyanja nyingine wanaweza kunufaika na kamusi hii katika kuelewa dhana zinazotumika katika uwanja huu, dhana ambazo huzisikia au kukutana nazo wanaposoma vitabu mbalimbali. Mwisho napenda kutoa wito kwa wataalamu wengine walio kwenye nyanja nyingine kuiga mfano ulioonyeshwa na Prof. Mwansoko na mwandishi mwenza Dkt. Mwita kwa kuunganisha nguvu za kitaaluma na kuweza kutoa kito hiki cha thamani. Ni imani yangu kuwa wataalamu wa fani tofauti tofauti wakiungana na wataalamu wa lugha wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, kazi ya kutunga kamusi za nyanja maalum itafanyika katika muda mfupi sana. Kwa utaratibu huo, tutaweza kujenga mazingira na msingi imara wa kukiwezesha Kiswahili kutumika kwa ufasaha katika taaluma mbalimbali. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili inawatakia wasomaji wote usomaji wenye manufaa. Tutashukuru sana kama tutapata maoni kutoka kwa wasomaji wetu ili tuweze kuyatumia katika kuiboresha kazi hii. Dkt. J.G.Kiango Kaimu Mkurugenzi Utangulizi Kamusi ya Tiba ni matunda ya juhudi za pamoja za wanaistilahi wawili na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Uandishi wa kamusi hii ulianza mwaka 1985 baada ya Dkt. Mwita kubaini kuwa kuna ombwe linalohitaji kuzibwa katika uwanja huu wa elimu. Mswada wa awali uliandikwa kwa hati ya mkono na kutokana na majukumu mengine, kazi hiyo ilifanyika kwa vipindi. Mswada ulichapwa katika kompyuta mwaka 1997 na hiyo ilirahisisha sana marekebisho mengi na makubwa yaliyofuatia. Mwaka 1998, Dkt. Mwita aliwasiliana na kuwasilisha mswada kwa Profesa Mwansoko wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Profesa Mwansoko alibaini kuwa mswada unafaa kuendelezwa zaidi hususan katika uundwaji wa istilahi sadifu zaidi. Aidha ni yeye aliyeandaa misingi na kanuni za uundaji wa istilahi za Kiswahili zilizotumiwa katika kamusi hii. Pia ndiye aliyeshughulikia lugha kienzo ya kamusi. Kazi hiyo nayo ilifanyika kwa vipindi kutokana na majukumu mengi ya kikazi ya waandishi wote wawili. Hatimaye mswada uliwasilishwa TUKI mwezi Juni, 2003 kwa uchapishaji. Hakika hii ilikuwa ni shughuli kubwa iliyochukua takribani miaka 18. Ni vyema kuwa TUKI imeafiki kuwa ni kazi nzuri inayostahili kuchapishwa. Waandishi wanaamini huu ni mwanzo wa safari ndefu katika kukuza lugha ya Kiswahili katika uwanja huu wa elimutiba. Uundaji wa istilahi za tiba si kazi rahisi. Ugumu wake unatokana na lugha ya kitabibu kutumiwa na kundi maalum la watu, yaani wataalam wa tiba. Hali hiyo inasababisha ukuzaji wa istilahi hizo katika lugha nyingine kuwa mgumu zaidi kwa kuwa si lugha ambayo hutumiwa na watu wa kawaida katika maisha yao ya kila siku. Aidha, kwa kuwa lugha hiyo haiko wazi kwa watu wengi, ni vigumu kupata visawe vya maneno mengi kutoka lugha kama vile Kiswahili, achilia mbali lugha za kikabila. Lugha ya kitabibu ina asili ya lugha nyingi, hususan, Kilatini, Kigiriki, Kijerumani, Kiingereza n. k. Lugha hizo zimekuwa zikitumika kuunda istilahi za tiba kwa miaka mingi, sambamba na ukuaji wa taaluma yenyewe kwa muda wa kame na kame. Ni matumaini ya waandishi kuwa kamusi hii itafungua ukurasa mpya kwa lugha ya Kiswahili nayo kutoa mchango wake katika uwanja huu. Nani anajua, huenda miaka ijayo ikawepo kamusi inayojitosheleza ya tiba ya Kiswahili- Kiingereza. Mchango mkubwa wa kuendeleza kamusi hii, kwa maana ya kukosoa na kuboresha zaidi istilahi zilizomo katika lugha ya Kiswahili au kikabila utatoka kwa watalaam mbalimbali wa tiba. Hakuna shaka, wataalam wa lugha ya Kiswahili wana nafasi maalum ya kuchangia katika uboreshaji wake. Ni matumaini ya waandishi kuwa toleo lijalo litakuwa bora zaidi. Licha ya waandishi kuunda istilahi, baadhi yake walizipata kutoka kwenye marejeo mbalimbali, zikiwemo kamusi. Kamusi zilizotumika ni pamoja na The Faber i Medical Dictionary (Faber and Faber Ltd, London 1975), Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford University Press, 1981), English-Swahili Dictionary (TUKI, 1996), Kamusi Sanifu ya Bilojia, Fizikia, na Kemia (TUKI 1990), Istilahi za UKIMWI (Baraza la Kiswahili la .Taifa-BAKITA, 2003). Vyanzo vingine ni mikutano na warsha mbalimbali ambazo Wizara ya Afya huwashirikisha watalaam kutoka BAKITA na TUKI. Aidha, maongezi ya kawaida na watu mbalimbali yamewasaidia waandishi kurutubisha istilahi zilizomo. Utohoaji wa maneno kutoka Kiingereza umefuata mtindo wa mifano michache ifuatayo: Kiambishi Utohoaji Maana Mfano a- - bila ya acatalasia-akatalasia: ukosefu wa enzaimu katalasi adeno- adeno- tezi adenopathy-adenopathi: ugonjwa wowote wa tezi -algia -aljia maumivu neuralgia- nuraljia: maumivu ya neva, ya vipindi an- an- upungufu anoxia-anoksia: upungufu wa oksijeni katika damu angio- anjio- mshipa angiospasm-anjiospazimu: mikazo ya mishipa ante- - kabla ya/mbele ya, ante-partum: kabla ya kuzaa anti- - zuia/tuliza/punguza, antispasmodic:kituliza spazimu auto- oto- -anafsia autophobia-otofobia: kujiogopa mwenyewe -cide -sidi -a kuua acaricide-akarisidi: dawa ya kuua kupe -dynia -dinia maumivu mastodyinia-mastodinia: maumivu ya matiti dys- dis- athari/matatizo dystocia-distosia: uchungu wa muda mrefu -genesis -jenesisi utengenezwaji lipp ogenesis-lipPoOj)e nesist: utengenezwaji wa mafuta hydro- hidro- -enye/-a kiowevu; hydroureter-hidroureta:kujaa kwa mkojo katika ureta -isis -isisi -a hali fulani; granulosis-granulosisi: uwepo wa granuli nyingi -itis -itisi inflamesheni otitis-otitisi: inflamesheni ya sikio li -Jojia tanzu ya elimu biology-biolojia: sayansi ya -logy viumbe hai -lisisi kusambaratika cytolysis-sitolisisi: -lysis kusambaratika kwa seli -pathi ugonjwa neuropathy- nuropathi: -pathy ugonjwa wowote ule wa neva -penia -penia upungufu leuupcoupnegnuifau- luwkao pleunkiosai:t i -pexy -peksi kutegemeza orchiopexy-okiopeksi: kutegemeza pumbu -phobia -fobia woga awcar okpihnoubriotai-kaik rowfao bkiiam:o wokigrae fu pio- usaha pyometra-piometra: pyo- mlundikano wa usaha katika uterasi -raphy -rafi ripea hoepmrieosrhernaip hyy-ah eknuiroirpaeaf i:h enia kupotea, kutokwa; pyorrhoea-piorea: kutoka -rrhoea Tea kwa usaha -scopy -skopi kutizama ; gastroscopy—gastroskopi: uchunguzi kwa kutizama tumboni chini ya subcutaneous-sabukteni: sub- sabu- chini ya ngozi -tomy -tomi kupasua, kukata; nephrotomy-nefrotomi: upasuaji wa figo -una -uria mkojo pkowlay urwiian-gpio lkiuurpiiat:a kkiuaksoi joa Vifupisho vifuatavyo vimetumika katika kamusi: adj - kivumishi adv - kielezi k. m. - kwa mfano k.v. - kama vile jina (nomino) n - nk. nakadhalika vy oO kitenzi ili Pamoja na juhudi zilizofanyika za kupitia kila ukurasa wa kamusi ili kuhakiki makosa, huenda toleo hili la kwanza bado linayo makosa ya hapa na pale. Makosa hayo yanaweza kuwa ya kiuandishi au vinginevyo. TUKI, kama wachapishaji, hawapaswi kulaumiwa kwa upungufu huo. Waandishi wanabeba dhamana hiyo na wanaomba radhi kwa hilo. La muhimu zaidi ni msomaji kuwasiliana na mchapishaji ili kuboresha toleo lijalo. Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wafuatao: Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya, nia na nguvu kwa kipindi hiki kirefu cha uandishi, kwa Sumiko Koga, mtaalam kutoka JICA ambaye mwaka 1997 alifanikisha upatikanaji wa kompyuta iliyotumika mwanzoni kwa ajili ya kazi hii, familia zetu kwa uvumilivu wao katika kipindi hiki kirefu, na TUKI kwa kukubali kuchapisha Kamusi hii. Tunahitimisha kwa kuwaomba watalaam wa tiba na watu wengine kwa ujumla watumie kamusi hii ya tiba na wachangie mawazo ambayo yataboresha toleo lijalo, siku za usoni. Hatua hii iliyopigwa ni ndogo sana kwani fani ya tiba ina marefu na mapana yasiyopimika. Aidha, tunaamini kuwa toleo hili ni changamoto ambayo itasaidia kupanua wigo wa kuendeleza lugha ya Kiswahili katika uwanja huu adimu. Dkt. A. M. A. Mwita (M.D, M. Sc.) Prof. H.J.M. Mwansoko (Dip. Journalism, Dip. Translation, M.A., Ph. D.) Dar es Salaam Desemba, 2003 iv

See more

The list of books you might like

Most books are stored in the elastic cloud where traffic is expensive. For this reason, we have a limit on daily download.